Wizkid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wizkid
Wizkid akitumbuiza katika tamasha la uzinduzi wa albamu ya Iyanya - Desire mnamo 2013
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaAyodeji Ibrahim Balogun
Amezaliwa16 Julai 1990 (1990-07-16) (umri 33)[1]
Surulere, Lagos, Lagos State, Nigeria
Kazi yake
  • Msanii wa rekodi
  • Mtunzi wa nyimbo
  • Mtumbuizaji
Miaka ya kazi2001–hadi sasa[2]
StudioYa sasa

Ya zamani

Ameshirikiana na

Ayodeji Ibrahim Balogun (amezaliwa 16 Julai, 1990), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Wizkid (wakati mwingine hupambizwa kama WizKid),[4] ni msanii wa rekodi, mtunzi wa nyimbo na mtumbuizaji kutoka nchini Nigeria. Alianza kazi ya muziki akiwa na umri wa miaka 11, na kutoa albamu ya ushirika akiwa na Glorious Five iliyopewa jina la Lil Prinz (2001). Mwaka wa 2009, ameingia mkataba na Banky W. iliyo chini ya Empire Mates Entertainment. Ameanza kupata umaarufu zaidi mnamo mwaka wa 2010 baada ya kutoa kibao cha "Holla at Your Boy" kutoka katika albamu yake ya kwanza iliyoitwa Superstar (2011). "Tease Me/Bad Guys", "Don't Dull", Gidi Girl, "Love My Baby", "Pakurumo" na "Oluwa Lo Ni" zilikuwa single kutoka katika albamu ya Superstar. Albamu yake ya pili iliyoitwa , Ayo (2014), ilitanguliwa na vibao kama vile "Jaiye Jaiye", "On Top Your Matter", "One Question", "Joy", "Bombay" na "Show You The Money". Kwa zaidi, katika kazi za kujitegemea, Wizkid amepata kushirikiana na baadhi ya wasanii ambao wamo katika kazi kama vile "Girl" (Bracket), "Fine Lady" (Lynxxx), "Sexy Mama" (Iyanya), "Slow Down" (R2Bees), "The Matter" (Maleek Berry), "Pull Over" (Kcee) na"Bad Girl" (Jesse Jagz).

Kazi na mchango wake katika Tasnia ya Muziki wa Nigeria umepelekea kupata mafanikio kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na tuzo ya BET Award, a MOBO Award, The Headies Awards tatu, Channel O Music Video Awards mbili, nne za Nigeria Entertainment Awards, Ghana Music Award, mbili za Dynamix All Youth Awards, mbili za City People Entertainment Awards, na Future Award. Kwa zaidi, amepata kuchaguliwa mara tatu katika MTV Europe Music Awards vilevile mara nne katika tuzo za World Music Awards. Alipata kuwa nafasi ya 5 kwa msanii mwenye pesa sana wa Afrika mwaka 2013 na jarida la Forbes na Channel O.[5][6] Mnamo Februari 2014, Wizkid amekuwa mwanamuziki wa kwanza wa Kinigeria kuvuka idadi ya milioni 1 ya watu wanaomfuta katika mtandao wa Twitter.[7][8]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Wizkid pops N300m champagne at 23rd birthday bash?". Punch Nigeria. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-10-29. Iliwekwa mnamo 9 Oktoba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Wizkid Biography". MTV Base. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-11-13. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Nissim, Mayer (11 Juni 2012). "Wizkid: 'Akon is like an older brother to me'". Digital Spy. Iliwekwa mnamo 7 Machi 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 "Artists – WizKid". Disturbing London. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-13. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Wizkid richer than 2Face, Banky W – Forbes". The City Reporters. 2 Septemba 2013. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Sarkodie Makes Forbes Top 10 Richest Africa Artistes". The Chronicle. 3 Septemba 2013. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "Wizkid- First Nigerian Artiste To Hit A Million Twitter Followers". Modern Ghana. 20 Februari 2014. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Guess Which Nigerian Artiste Becomes The First To Gain 1 Million Followers on Twitter". Naij News. 20 Februari 2014. Iliwekwa mnamo 5 Machi 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Kigezo:Empire Mates Entertainment Kigezo:Konvict Muzik