Mshambuliaji wa Aljeria Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka baada ya kuiwezesha klabu yake ya Leicester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita. Nenda kwenye makala
Bonyeza hapa kusoma Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW
Wawakilishi wa makabila mawili nchini Namibia wamefungua kesi katika mahakama nchini Marekani dhidi ya Ujerumani wakidai fidia kwa madai ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na watawala wa zamani wa wakoloni wa kijerumani.
Wakuu wa mashirika ya ujasusi nchini Marekani wanatazamiwa kumkabidhi rais mteule Donald Trump maelezo ya kina juu ya ushahidi walioukusanya kwamba Urusi ilifanya jitihada za kuvuruga uchaguzi wa taifa hilo na udukuzi.
Mkuu wa majeshi ya Gambia, Luteni Jenerali Ousman Badjie, amerudia kuelezea hatua yake ya kumtii kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Yahya Jammeh, licha ya kushindwa uchaguzi mwaka jana. Hatua ya kiongozi huyo wa kijeshi kumuunga mkono Jammeh inaongeza mvutano katika nchi hiyo iliyogawanyika. Sikiliza mahojiano haya na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Tanzania, Bashiru Ali, akifafanua.
Wafanyakazi 400 wa Uganda wameanza mgomo wakilalamikia unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mameneja wa kampuni ya Kichina wanayoifanyia kazi mjini Kampala.
Ilhan Omar wa chama cha Democrat anakuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuapishwa kuwa mbunge akiliwalikisha jimbo la Minnesota linalokaliwa na Wasomali wengi zaidi Marekani.
Waasi nchini Msumbiji wametangaza kurefusha kwa miezi miwili makubaliano ya kusitisha vita baina yao na serikali na kuongeza matumaini ya kupatikana kwa amani baada ya machafuko ya mwaka jana kugharimu maisha ya watu.
Zaidi ya wasichana 800 walikeketwa kaskazini mwa Tanzania Desemba 2016 licha ya jitihada kadhaa za polisi dhidi ya vitendo hivyo. Ni kitu gani kinachangia kuendelea kwa vitendo hivyo nchini Tanzania? Msikilize Zainab Aziz akimhoji Eddah Sanga mkurugenzi mtendaji wa shirika la waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA.
Madaktari nchini Ujerumani wamewashauri raia kutembea kama ndege aina ya Penguin kwa lengo la kuepuka kuteleza na kuanguka katika kipindi hiki cha baridi jambo linalotokana na kuganda kwa barafu baraabarani.
Wakati kwenye jamii nyingi duniani, mtu mjinga hufananishwa na kuku, wanasayansi wanasema ukweli ni kuwa kuku ndiye ndege mwenye akili zaidi kuliko ndege wote ulimwenguni.
Mwimbaji wa muziki wa "pop" nchini Marekani, Janet Jackson, amejifunguwa mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50, kwenye ndoa yake ya tatu na bilionea wa Qatar, Wassim al-Mana.
Bwana mmoja mwenye umri wa miaka 54 nchini Vietnam, Man Van Nhat ameondolewa kifaa cha upasuaji kilichosahahulika wakati wa akifanyiwa operesheni tumboni mwake kwa miaka 18 iliyopita.
Sikiliza shindano hapa kisha utume jibu lako sahihi ili kupata nafasi ya kushinnidia zawadi kemkem
Ligi kuu ya kandanda hapa Ujerumani iko katika kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi na baada ya kuwa na likizo fupi ya sherehe za Krismasi timu zimeanza leo kuyaoa makali
Tuma Facebook Twitter Google+ Whatsapp Tumblr Digg Newsvine
Kiungo http://dw.com/p/2VPjq
Afisa wa juu kabisa wa ujasusi Marekani amesema ana imani kuwa Urusi imedukua uchaguzi wa taifa hilo, Ujerumani imeshitakiwa kwa mauwaji ya halaiki Namibia na Mshambuliaji wa Algeria Riyad Mahrez ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka barani Afrika
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com
Kiungo http://dw.com/p/2SSau
Dar es Salaam, jiji kuu la kiuchumi na kibiashara nchini Tanzania, Mohammed Khelef alikutana na vijana wanaoshajiisha na kujihusisha na ujasiriamali jamii kupitia mitandao ya kijamii inayowakutanisha na mamilioni ya wenzao kote duniani
Kiungo http://dw.com/p/2SSbU
Nini nafasi ya mitandao hii kwenye kubadili maisha ya vijana wa Kiafrika na kuwafanya kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha yao? Mjini Nairobi, Mohammed Khelef alikutana na mwanablogu maarufu Robert Alai, na hapa anazungumzia kile ambacho mitandao ya kijamii inamaanisha kwake na kwa jamii ya vijana wa Kenya
Kiungo http://dw.com/p/2SSbX
Mohammed Khelef akutana na vijana wa jijini Nairobi wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasishana katika kilimo salama kwenye maeneo ya mijini kupitia kampeni wanayoiita “Adilisha“
Kiungo http://dw.com/p/2SSbZ
Shirika la Jamii Media ambalo linaendesha mtandao wa kijamii wa Jamii Forum linasimamia hivi sasa mradi wa kufuatilia utekelezaji ahadi za wanasiasa waliochaguliwa kwa kura majimboni kwa kutumia mitandao ya kijamii unaoitwa Tushirikishane
Kiungo http://dw.com/p/2SSbV
Katika mji wa kitalii wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, vijana wanaotokea asasi za kijamii na za kibiashara zinazoyalenga makundi maalum ya kijamii, mitandao ya kijamii imekuwa kila kitu kuhusu maisha yao
Kiungo http://dw.com/p/2Sicr
Mitandao ya kijamii inajenga mtandao baina ya watu na inawaleta karibu zaidi hata wale walio mbali.
Kiungo http://dw.com/p/2SSbW
Mwenzangu Mohammed Khelef amezungumza na George Akilimali, mwanzilishi wa Kampuni ya SmartCore Social Enterprise, inayojihusisha na uwezeshaji wa vijana katika kuifikia teknolojia, jijini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, juu ya dhana ya "uchumi wa mitandao ya kijamii".
Kiungo http://dw.com/p/2Sp03
Alama unazowacha mtandaoni ni tafsiri inayoelezea wewe ni nani na watu huenda wakakutafsiri kwa alama hizo.
Bonyeza hapa kupata mukhtasari wa habari muhimu duniani katika video fupi za 'Papo Kwa Papo'